Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje kufahamu
OFISI INAYOHUSIKA
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Urasimishaji rasilimali vijijini ni utaratibu unaowezesha kutoka kwenye umiliki usiokidhi matakwa ya kisheria kuwa na umiliki ulio rasmi unaozingatia utawala wa sheria. Hatua zifuatazo huzingatiwa katika urasimishaji rasilimali vijijini kama ilivyoainishwa katika sheria husika:

 

 • Kuhakikisha mipaka ya kijiji imehakikiwa na kupimwa ipasavyo ili kuepusha migogoro
  ya mipaka na vijiji jirani
 • Kusajili na kupata Cheti cha Ardhi ya Kijiji
 • Kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji
 • Kijiji kuwa na jengo linalofaa kwa ofisi ya Masjala ya ardhi ya Kijiji
 • Kutuma maombi ya kupimiwa na kupata hati miliki ya kimila kwenye Halmashauri ya
  Kijiji kwa ajili ya mapendekezo ya kuidhinishwa
 • Mkutano Mkuu wa  Kijiji kupitisha na kuidhinisha maombi ya kupimiwa na kupatiwa
  Hati Miliki ya Kimila
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 27-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page