Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kutoa Malalamiko
OFISI INAYOHUSIKA
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Kupokea malalamiko yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora ni moja kati ya kazi muhimu za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), kama inavyobainishwa katika kifungu cha 6(1) cha Sheria Na. 7 ya mwaka 2001 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Kazi nyingine inayoambana na hii ni kuyafanyia uchunguzi malalamiko yanayopokelewa na kutoa mapendekezo. Huduma hii inatolewa bure.

Malalamiko yanaweza kuwasilishwa na mtu mmoja, kikundi cha watu au taasisi kwa: Kuandika baruakufika kwenye mojawapo ya ofisi za Tume na kutoa maelezo na kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani (SMS) kwenda Na. 0754 460 259 ukianza ujumbe wako na neno: “TAARIFA” au “REPORT”.

Mahitaji:

 • Barua yenye maelezo yanayojitosheleza kuhusiana na lalamiko.
 • Mwandishi wa barua aandike jina kamili, anwani yake, namba ya simu na anwani ya barua pepe (kama anazo).
 • Mlalamikaji ataje jina na anwani ya mtu, taasisi au mamlaka anayoilalamikia.
 • Mlalamikaji aweke nakala (photocopies) za nyaraka muhimu – mfano, barua ya ajira/kupandishwa cheo kwa masuala yanayohusiana na ajira.

Utaratibu:

 • Kutegemeana na mahali ulipo, tuma barua yako kwa kutumia mojawapo ya anuani zifuatazo.
 • Fika kwenye kwenye mojawapo ya ofisi za Tume.

Kumbuka:

 • Anuani/mawasiliano kamili ya mlalamikaji na mlalamikiwa ni muhimu ili Tume iweze 
  kuendeleza mawasiliano na pande zote mbili.
 • Iwapo umetuma lalamiko lako kwa SMS, utajulishwa juu ya kupokelewa kwa
  lalamiko lako kupitia namba ya simu uliyoitumia kutuma lalamiko lako. 
 • Lalamiko lako litakapoanza kushughulikiwa utapata ujumbe kujulishwa
  namba ya lalamiko, ambayo utaitumia kufuatilia lalamiko lako.
 • Taarifa za kupokelewa kwa lalamiko na namba ya lalamiko zitatumwa pia kwa njia ya barua.
 • Namba 0754 460 259 inapokea ujumbe tu, hivyo usipige simu kwenda
  namba hii, haitapokelewa. 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 20-12-2016
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page