Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje kufahamu
OFISI INAYOHUSIKA
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Urasimishaji rasilimali mijini ni utaratibu unaowezesha kutoka kwenye umiliki wa rasilimali zilizoko mijini usiokidhi matakwa
ya kisheria kuwa na umiliki ulio rasmi unaozingatia utawala wa sheria. Hatua zifuatazo
huzingatiwa katika urasimishaji rasilimali mijini kama ilivyoainishwa katika sheria husika kama

vile Sheria ya Ardhi Na. 4 ya 1999 na Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya 2007:

  • Kutambuliwa na kuainishwa kwa eneo la urasimishaji na Halmashauri husika katika
    mji, Manispaa au Jiji,
  • Uhamasishaji kwa Uongozi na wananchi wa eneo la urasimishaji,
  • Utayarishaji wa michoro ya mipango miji na kuidhinishwa na mamlaka husika,
  • Upimaji ardhi ya wananchi kulingana na michoro ya mipango miji
  • Uidhinishaji wa ramani za upimaji kwenye mamlaka husika,
  • Utayarishaji na utoaji wa Hati za kumiliki ardhi kwa wamiliki wa ardhi iliyopimwa.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 30-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page