Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje kufahamu
OFISI INAYOHUSIKA
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

MKURABITA ni nyenzo ya kuwawezesha watanzania kiuchumi kwa kutumia vipaji, rasilimali na biashara zao zinazotambulika kisheria katika kujipatia mitaji. MKURABITA imebuni utaratibu wa kujenga uwezo wa walengwa kutumia mali zao zilizorasimishwa katika kujipatia mitaji. Lengo la kuwajengea uwezo walengwa ni pamoja na kuwawezesha  kuelewa juu ya:

 • Utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu ya biashara
 • Kuandaa mpango wa biashara
 • Taratibu za mikopo kutoka taasisi za fedha
 • Kufungua na kutuza akaunti mbalimbali kutoka kaika taasisi za fedha

Shughuli zinazofanyika:

MKURABITA kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa, taasisi za fedha na halmashauri
husika hufanya uhamasishaji kwa wananchi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha yafuatayo 
yanatekelezwa:

               i.        Kujenga uwezo wa wafanya biashara

              ii.        Kuwaunganisha wafanya na taasisi za fedha pamoja  huduma za mifuko ya hifadhi ya jamii .

             iv.        Kujenga uwezo wa wamiliki wa rasilimali

              v.        Kuwaunganisha wamiliki wa rasilismali na taasisi za fedha, bodi za mazao na mifuko ya  hifadhi ya jamii

            vii.        Kujenga uwezo wa vyama vya wafanya biashara na wakulima ikiwemo VIBINDO, VICOBA na ITOA

             ix.        Kurahisisha upatikanaji wa huduma za mikopo, pembejeo na ushauri wa kitaalam

              x.        Kutoa mafunzo yanayohusiana na masuala ya:

             xi.        Huduma za kibenki

  • Utunzaji wa fedha
  • Utoaji na ulipaji wa mikopo
  • Utumaji wa fedha ndani na nje ya nchi
  • Ulipaji wa Ankara
  • Uthamini wa mali
  •  Kuendesha Biashara Rasmi
   • Kutunza kumbukumbu za mahesabu ya biashara
   • Kuandaa mpango wa biashara
   • Kuandaa mpango wa mtiririko wa fedha
  •  Kupata na kuongeza mitaji
   • Kubaini fursa za kupata na kuongeza mitaji
   • Kubaini na kupata mbia
   • Kukodi mali iliyorasmi
   • Kutafuta mwekezaji
   • Kuuza mali kwa tija/faida kubwa

Manufaa:

 • Utaratibu huu wa kujenga uwezo wamiliki wa rasilimali na biashara ni shirikishi
 • Unarahisisha kuziunganisha mali zilizorasimishwa na fursa za kiuchumi
 • Wananchi waliorasimisha mali zao wameanza kunufaika na huduma za ukazaji wa
  mitaji
 • Utaratibu huu shirikishi kijamii na kiuchumi umepokelewa na unakubalika na wadau 
  mbalimbali wameanza kushirikiana na MKURABITA na halmashauri.

       i.      

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 26-01-2017
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page