Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Mapato Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Wakala wa Utoaji na Usafirishaji wa Mizigo ni watu waliopewa leseni na kamishna wa idara ya ushuru na forodha kufanya kazi ya kushughulikia nyaraka na kutoa mizigo kutoka kwenye uthibiti wa forodha kwa niaba ya waagizaji kutoka nje.

Masharti:

 • Awe na angalau wafanyakazi wawili watakaohusika na utoaji wa mizigo na wenye uzoefu usiopungua miaka mitano katika shughuli za forodha
 • Wafanyakazi hao wawe na angalau diploma/cheti cha mafunzo ya forodha
 • Awe na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN)
 • Uthibitisho wa uhusikaji/uanachama wa chama cha utoaji na usafirishaji wa mizigo
 • Asiwe ametelekeza PADS/Makosa au dhima nyingine zozote anazodaiwa na TRA
 • Cheti cha usajili na SUMATRA
 • Maelezo ya akaunti ya benki
 • Cheti cha VAT
 • Barua ya uthibitisho wa kulipa kodi kutoka idara ya kodi ya ndani/walipaji wakubwa wa kodi, leseni halali ya biashara kutoka wizara ya viwanda, biashara na masoko
 • Katiba na kanuni za kampuni
 • Cheti cha uandikishaji/usajili
 • Leseni halali ya forodha ya mwaka uliopita
 • Picha za pasipoti za hivi karibu za wakurugenzi na wafanyakazi muhimu
 • Nakala za kitambulisho, pasipoti/aina nyingine za utambulisho wa wafanyakazi
 • Hati ya kukodi/hatimiliki ya ofisi/jengo
 • Barua kutoka wadhamini waliothibitisha uwasilishaji wa malipo ya mwaka kuhusiana na dhamana mbalimbali
 • Mikataba halali ya kupanga ofisi inayofaa/uthibitisho wa umiliki

Taratibu:

 • Omba kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Maombi ya Leseni ya Forodha
  (CULAS)
 • Ambatisha nyaraka kama zilivyotajwa kwenye masharti
 • Lipa Dola za Marekani 50 kama ada ya maombi
 • Onyesha uthibitisho wa ushirikishwaji/uanachama wa chama cha utoaji na
  usafirishaji mizigo kinachotambulika
 • Wasilisha maombi yako kwa Idara ya Kamishna wa Forodha na Ushuru

Zingatia: 

 • Wafanyakazi wa TRA hawastahili kuwa na hisa yoyote kwenye utoaji na
  usafirishaji wa mizigo

 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page