Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba
OFISI INAYOHUSIKA
Wizara ya Viwanda na Biashara

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Dalali ni mtu au kampuni inayofanyakazi kama chombo cha kati ya mnunuzi na mwuzaji, kwa kawaida anatoza kamisheni. Kutokana na sababu hii akaunti ya udalali ni utaratibu kati ya mwelekezaji na kampuni ya udalali iliyosajiliwa inayomwezesha mwekezaji kuweka fedha katika kampuni  na kuingiza maagizo ya uwekezaji kupitia udalali, ambao baadae hufanya miamala kwa niaba ya mwekezaji.

Masharti:

  • Nakala ya pasipoti yako/ kitambulisho au leseni ya udereva.
  • Lipa ada iliyoelekezwa.

Taratibu:

  • Kamilisha Fomu ya Kufungulia Akaunti ya Mfumo mkuu wa uwekaji (CDS).
  • Irudishe kwa dalali wako ili ipewe namba ya akaunti ya CDS.
  • Kamilisha fomu ya kufungulia akaunti ya Dalali
  • Ambatisha nakala yako ya pasipoti/ kitambulisho/ leseni ya udereva
  •  Mtumie dalali wako nakala halisi ya fomu ya CDS.
  • Tuma fedha kwa mtandao kwenye akaunti yako ya udalali
  • Wasilisha agizo la biashara.

Zingatia:

  • Haiwezekani kuweka gawio la hisa moja kwa moja kwenye akaunti ya udalali ya Tanzania. Badala yake ukubali kupokea gawio kwa fedha za Tanzania.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page