Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Mapato Tanzania

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Leseni ya udereva ni waraka rasmi unaoeleza kuwa mtu anaweza kuendesha chombo cha moto, kama vile pikipiki, gari dogo, lori au basi, katika barabara ya umma. Wenye leseni za udereva za baadhi ya daraja watalazimika kuendesha daraja hiyo baada ya kujaribiwa na si vinginevyo.

Masharti:

 • Amehudhuria chuo chochote cha udereva kinachotambuliwa na kupata cheti
 • Umri unaozidi miaka 18 kwa gari na miaka 16 kwa pikipiki
 • Uwe na leseni ya muda/kujifunzia udereva (Tsh.10,000/= inaongezwa muda kila miezi mitatu)
 • Lazima ulipe ada ya kupimwa –GRR
 • Lazima uwe na cheti cha kipimo cha macho
 • Lazima uombe Idara ya Usalama Barabarani kwa kujaribiwa
 • Lazima uende Idara ya Usalama Barabarani na gari kwa ajili ya kujaribiwa
 • Lipa ada ya Tsh.3,000 ya majaribio ya udereva
 • Mwombaji akishajaribiwa anaweza kuruhusiwa kuendesha pikipiki na gari ndogo

 

Taratibu:

 • Jaza fomu ya kupewa namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) (iwapo hujakuwa nayo)
 • Jaza fomu ya leseni iliyoelezwa katika mamlaka ya kodi Tanzania
 • Lipa ada ya leseni iliyopendekezwa ya Tsh. 40,000/= kupitia benki
 • Taarifa zako zote zitaingizwa kwenye mfumo wa kompyuta kwa ajili ya kukusanya data
 • Polisi watakupa nyaraka za kupeleka TRA
 • TRA itakupatia leseni ya udereva

Zingatia:

 • Leseni itakuwa kwa mtindo wa kadi ngumu kama za benki na nembo ya bendera
  ya taifa
 • Makosa yote yatakayofanywa na dereva yatabainishwa kutokana mfumo huu mpya wa
  leseni.
 • Leseni inaweza kusitishwa au kuchukuliwa kutegemea uzito wa makosa
 • Leseni ya udereva itakuwa halali kwa kipindi cha miaka mitatu na utatakiwa
  kuiongeza muda wa matumizi
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page