Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Vyeti
OFISI INAYOHUSIKA
Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Cheti cha kuzaliwa ni waraka muhimu na halisi unaoandikwa kwenye rejesta ya vizazi ya nchi alikozaliwa mtoto. Cheti hicho kina taarifa kama vile mahali, mwaka, mwezi, siku, tarehe na wakati alipozaliwa motto. Waraka huu ni muhimu na wenye manufaa ni utambulisho wa kujua utaifa na umri wa mtu.

Masharti:

  • Picha tatu za pasipoti
  • Uwe na angalau kimojawapo kati ya hivi: kadi ya kliniki, cheti cha ubatizo, cheti cha kumaliza shule (msingi/sekondari)

Taratibu:

  • Peleka maombi kupitia barua pepe ya RITA (info@rita.go.tz)
  • Jaza Fomu na kuwasilisha kupitia barua pepe
  • Ambatisha angalau kimojawapo kati ya hivi: kadi ya kliniki, cheti cha ubatizo, cheti cha kumaliza shule (Msing/ Sekondari)
  • Pokea barua pepe kutoka RITA, pamoja na kiambatisho cha Fomu ya Kiapo, halafu ambatisha na nakala tatu za picha za pasipoti
  • Skani fomu ya kiapo na itume kupitia barua pepe
  • Pokea barua pepe kutoka RITA, inayoruhusu kuendelea na mchakato wa malipo
  • Lipa cheti cha mtoto kilichoelezwa chini ya umri wa miaka 10 – dola za Marekani 14, zaidi ya miaka 10 na kuendelea , Dola za Marekani 20. Na kupitisha Hundi – Dola za Marekani 20.
  • Malipo ni lazima yafanywe kupitia DHL-EMS n.k
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page