Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kuomba PasiPoti/Pasi/Visa
OFISI INAYOHUSIKA
Uhamiaji

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Ni hati inayotolewa na serikali ili kumwezesha raia wake aweze kusafiri nje ya mipaka ya nchi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi anayokwenda au kupitia. Licha ya kuwa pasipoti hutolewa kwa jina na maelezo mengine yanayomhusu mwombaji,hati hiyo hubaki kuwa ni mali ya serikali.

Masharti:

 • Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa.
 • Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa cha
  mzazi au wazazi
 • Picha sai ya hivi karibuni ya pasipoti isiyo kwenye fremu.
 • Iwapo mwombaji ana umri wa chini nya miaka kumi na nane (18), wazazi/
  walezi wawasilishe ridhaa ya maandishi.

Taratibu:

 • Jaza Fomu ya Maombi iliyoelezwa katika ofisi ya uhamiaji.
 • Wasilisha fomu ya maombi kwa mkurugenzi wa uhamiaji.
 • Wasilisha nyaraka zote zinazotakiwa kama ilivyoelezwa hapo juu.
 • Lipa ada ya Tshs 50,000/= kama ilivyoelekezwa.

Zingatia: Mbali na masharti hayo ya jumla yapo maelelzo ya viambatanisho maalum kutokana na aina ya safari kama ilivyoainishwa nyuma ya fomu ya ombi la pasipoti.

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page