Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kupata Leseni
OFISI INAYOHUSIKA
Mamlaka ya Chakula na Dawa

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Famasia ni duka linalotoa na kuuza dawa za tiba.  Kwa hiyo, nchini Tanzania, leseni ya uuzaji wa dawa inatolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na mtengenezaji kuwa na leseni ya bidhaa iliyotolewa na Mamlaka kama ilivyoelezwa na Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2003.

Masharti:

 • Hakikisha kuwa umesajiliwa katika TFDA.
 • Lipa ada iliyoelezwa.
 • Hakuna mtu atakayeruhusiwa kutengeneza na kuuza bila kibali.
 • Hairuhusiwi kugawa au kuhifadhi bidhaa mpaka uwe umesajiliwa.

Taratibu:

 • Omba kwa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA.
 • Peleka nakala kwa Mkaguzi wa eneo linalokusudiwa kufunguliwa biashara.
 • Muone Mkaguzi akakague eneo/jengo la biashara yako.
 • Wasilisha ripoti kwa uthibitisho TFDA.
 • Iwapo itathibitishwa, lipa ada iliyoelezwa.
 • Chukua cheti cha usajili kutoka TFDA.

 

Zingatia:

 • Leseni huongezwa muda kila mwaka ifikapo tarehe 1 Julai.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015
 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page